Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Laurent Samatta/Risasi
NGULI wa filamu za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’, amesema kuwa pamoja na kuendelea kulia juu ya kuibiwa kazi zao, anamkumbusha Rais Jakaya Kikwete kutimiza ahadi yake aliyowahi kusema kwenye msiba wa nguli wa filamu, Steven Kanumba kuwa atawashungulikia wale wote wanaoiba kazi za wasanii na kutoa kopi.

Nguli wa filamu za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’.
JB alitoa ombi  kwa uchungu ambapo alifunguka kuwa pamoja na kuwepo kwa wasambazaji lakini bado wasanii wamekuwa wakilia kila siku hasa pale wanapopeleka filamu zao sokoni.
“Rais wetu alitoa kauli kuwa anawashungulikia wale wote wanaohusika na wizi wa kazi zetu, lakini hadi leo bado hajatekeleza hilo, lakini hatuwezi kushindwa kusema kuwa tunaumia sana, tunaomba atusaidie,” alisema JB.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top