Zikiwa ni siku 10 tangu Bobbi Kristina apoteze fahamu na kuendelea kutumia mashine zinazomsaidia kupumua hadi sasa imeelezwa hali yake bado haijabadilika tangu adondoke bafuni na kukimbizwa katika hospitali ya Emory University hospital iliyopo Atlanta, Marekani.
Kwa mujibu wa familia ya Kristina na madaktari wamekubaliana kumwondolea mashine anayopumulia kesho ikiwa ni siku ambayo mama yake mzazi Whitney Houston alifariki dunia katika mazingira ya kudondoka bafuni kama mtoto wake.

Baba yake Kristina, Bobby brown akitoka hospitali
Madaktari wameonyesha kukata tamaa ya kurejesha tena maisha ya mtoto huyo na kuamua kuiachia familia juu ya hatma ya mtoto wao kufanya maamuzi kuhusu kutoa mashine anayopumulia.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment