June 21, 2025 03:44:08 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Watu wanaolala kwa zaidi ya masaa manane kwa siku wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kiharusi,utafiti umesema lakini wataalam hawajui sababu yake.

Utafiti uliofanywa kwa takriban watu 10,000 katika chuo kikuu cha Cambridge ulibaini kwamba wale wanaolala kwa takriban saa nane wana uwezekano mkubwa wa asilimia 46 kupata kiharusi.

Watu wazima hupendelea kulala kati ya saa sita na tisa ili kupumzika vizuri,lakini kulala zaidi hushirikishwa na matatizo ya afya kama vile ugonjwa wa sukari pamoja na ule wa kunenepa kupitia kiasi.

Hatahivyo haijabainika kutoka kwa utafiti huo iwapo kulala kwa zaidi ya saa nane huenda ndiko kunakosababisha matatizo hayo ambayo husababisha kiharusi ama iwapo ni miongoni mwa sababu za magonjwa yasiyojulikana.

Utafiti huo ulifanywa miongoni mwa watu walioko na kati ya miaka 42 na 81.

Watafiti walichunguza mienendo yao ya kulala kwa kipindi cha miaka 10 ambapo watu 346 walipatwa na kiharusi.

Baada ya kuangazia athari kama vile miaka na jinsia, watu waliosema wamekuwa wakilala kwa zaidi ya masaa manane walipatikana na hatari ya asilimia 46 kupatwa na ugonjwa huo.

Wale walioweza kulala kwa chini ya masaa sita walipatikana na hatari ya asilimia 18

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
28 Feb 2015

Post a Comment

 
Top