Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa.
Miss Tanzania wa mwaka 2013, Happiness Watimanywa amesema kuwa mashindano ya Miss Tanzania yana kasoro kubwa na kwamba mwaka jana hakutegemea kushinda, lakini alishangaa kutangazwa kuwa mshindi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Watimanywa amesema kina dada ambao wanatarajia kuwa mamiss wataumia kutokana na kusimamishwa kwa mashindano ya Miss Tanzania baada ya kutokea kasoro mashindano ya mwaka jana.

Hivi karibuni Serikali ya Tanzania iliyafungia kwa miaka miwili mashindano ya Miss Tanzania baada ya waandalizi kudaiwa kukiuka taratibu na kanuni katika mashindano ya Miss Tanzania 2014.

"Nilishangaa kutangazwa kwamba nimeshanda na kuwa Miss Tanzania Mwaka 2013, mimi sikustahili kushinda kwa sababu kulikuwa na warembo zaidi yangu," amesema Watimanywa.


Chanzo: Star TV

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top