Akizungumza na mwandishi wetu Veronica alisema mwanaye Suleiman Abdallah (4), alipozaliwa tu, choo chake hakikutoka kwa njia ya kawaida bali kilitokea mdomoni huku manesi wakisema ana utumbo mkubwa na moja kwa moja alichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na hali yake kuwa mbaya.
“Tulipofika pale Muhimbili mwanangu aliwekewa mashine ya kupumulia na baada ya kumchukua vipimo waligundua kuwa utumbo mkubwa wa choo umejifunga wakasema itabidi alazwe kwa ajili ya upasuaji ambapo alipasuliwa na kuwekewa utumbo wa plastiki ambao anaishi nao mpaka leo.
“Sasa tukaandikiwa tuwe tunahudhuria kliniki kila mwezi kutokana na tarehe husika lakini mwezi uliopita mtoto alianza kulalamika kuwa anasikia maumivu makali ya tumbo na hapati choo kabisa na hata akipata ni kidogo sana.
Mama huyo anaelezea kuwa yeye ndiye mlezi wa mtoto huyo baada ya kutelekezwa na mzazi mwenzie ambaye alidai hajali kumhudumia.
“Baba wa mtoto alipoona mwanaye ana matatizo haya alisema hanihitaji mimi na mtoto niende nikatafute mtu wa kunisaidia na yeye atatafuta mwanamke mwingine wa kuzaa naye pia nilishawahi kupigwa na shangazi yake kwa madai kuwa namsumbua mwanaye.
“Nimekuwa nikihangaika mwenyewe kwa miaka yote tangu alipozaliwa na tayari ameshapasuliwa mara nne tangu azaliwe lakini bado tatizo linaendelea kumtesa mtoto.
“Kwa sasa naomba serikali inisaidie kama inawezekana naomba mwanangu achunguzwe tena kwa sababu sasa hivi analalamika sana na hata tumbo lake linajaa,” alisema na kuongeza kuwa ili apasuliwe tena zinahitajika fedha shilingi 1,000,000 ambazo hana hata senti tano.
Aliyeguswa na kuhuzunishwa na mateso ya mtoto Suleiman anaweza kuchangia kupitia namba ya simu 0712 004 677 na 0767 026 551.
Post a Comment
Post a Comment