Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Nchini marekani huwa hakuishi vituko hasa miongoni mwa wasanii ambao siku zote wamekuwa wakipenda kuzungumzwa kwenye vyombo vya habari huku ikiaminika kuwa kuzungumzwa sana ndio hasa kinachowaongezea umaarufu. 

Hali hii imeonekana wazi baada ya rapa asiyejulikana sana Kevin Gates kukiri kufanya mapenzi na msichana ambaye amekuja kugundua kuwa ni ndugu yake wa damu . 

Kevin Gates akitumia ukurasa wake binafsi wa mtandao wa kijamii wa Instagram alikiri kufanya mapenzi na ndugu yake wa damu baada ya kuthibitishiwa na bibi yake na pamoja na kugundua hivyo rapa huyo amesema kuwa hana mpango wa kuachana na binti huyo na uhusiano uliopo baina yao utaendelea. 

Msaniii huyu wa muziki wa Hip-Hop amekiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na ndugu yake wa damu. 

Gates alipost video ambayo alikiri kuwa na uhusiano na binti ambaye baadaye alikuja kuambiwa kuwa ni ndugu yake , na maneno yalikuwa haya … 

’siwezi kumuacha msichana huyu kwani ananiridhisha kimapenzi na hata kama ni ndugu mimi sikukua pamoja na yeye tumekutana ukubwani tu na siwezi kumuacha hata kama ni ndugu yangu wa damu siwezi kuzuia kitu kizuri kinachoendelea kati yetu’..Alisema rapa huyo. 

Gates amesema kuwa hatasitisha uhusiano wake na binamu yake kwani haoni tatizo lolote

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top