
Simon Msuva kweli sasa yuko on fire, amepiga bao tatu, hat trick wakati Yanga ikiimaliza Taifa Jang'ombe kwa mabao 4-0.
Katika mechi hiyo ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar, bao moja lilifungwa na Mliberia, Kpah Sherman.
Yanga ndiyo ilitawala zaidi mchezo huo licha ya Taifa kucheza kibabe sana.
Kasi ya Yanga ilionyesha kuwazidi vijana hao wa Jang'ombe na Yanga wangekuwa makini zaidi, basi ingekuwa mvua ya mabao.
Mechi nyingine:
Azam FC imeanza michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa sare ya mabao 2-2.
Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Azam FC walianza kupata bao kupitia nahodha John Bocco, KCCA wakasawazisha na baadaye Salum Abubakari ‘Sure Boy’ akafunga tena, Waganda wakasawazisha tena.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment