Bao pekee la ushindi kwa Mtibwa Sugar limefungwa na kiungo wa zamani wa Simba na nahodha wa Taifa Stars, Henry Joseph Shindika katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza.
Katika mechi hiyo, wachezani wanne wa kigeni wa Simba, Juuko Musheed, Joseph Owino, Simon Sserunkuma na Emmanuel Okwi hawakuwepo kikosini.
Danny Sserunkuma pekee ndiye alikuwepo, hata hivyo alianzia benchi na alipoingia alijitahidi kutafuta bao la kusawazisha, lakini malengo yake yaligonga mwamba.
Wakati huo huo, Kocha mkuu mpya wa Simba sc, Goran Kapunovic aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja mchana wa leo alihudhuria mechi hiyo iliyopigwa uwanja wa Amaan Unguja.
Mechi hiyo ilitanguliwa na mechi mbili ambapo JKU waliitandika mabao 2-0 Mafunzo, zote za Zanzibar. Mechi ya pili Shaba iliitandika baoa 1-0 Polisi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment