Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Mwanaume mmoja Brazil amewashangaza wengi baada, ameweza kutembea masaa mawili kuelekea hospitali akiwa na kisu kichwani alichochomwa na majambazi waliomvamia akiwa anatoka Club. 
Kisu hicho kilizama kichwani kwa urefu wa 30cm kilimpata mwanaume huyo Juacelo Nunes pembeni ya jicho la kushoto na kutokea kwenye shavu wakati akipambana na majambazi hao.
“Kisu kilipita katika baadhi ya mishipa yake ya damu ambayo ingeweza kumuua kutokana na kuvuja kwa damu nyingi,” alisema daktari Gilberto Albuquerquealiyemhudumia mgonjwa huyo kutoka hospitali ya Teresina alipofikia kupata matibabu.
Kisu hicho kilitolewa na kukabidhiwa Polisi ambao wanaendelea na uchunguzi kuwatafuta wahusika wa tukio hilo. 


Daktari amesema mgonjwa huyo kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa madaktari na hali yake inaendelea vizuri.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top