Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe ‘Wolper’ ameamua kuanika ukweli kuwa sasa hivi anataka kuwa fundi wa kushona nguo ili kuepukana na ‘masnichi’ waliopo kwenye tasnia ya uigizaji.

Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe ‘Wolper’ akipozi.
Akizungumza na Amani, Wolper alisema ameamua kujikita huko kwa sababu ameona Bongo Movie hakuna maendeleo zaidi ya umbeya na hata soko la filamu linazidi kushuka.“Mimi ni msanii wa muda mrefu sana na kwa kazi ambazo tayari nimeshazifanya tangu kipindi hicho mpaka sasa naona tasnia haina maendeleo bali wamejaa masnichi tu yaani umbeyaumbeya tu.” 
“Ni bora niwe fundi nguo ili kuepukana na manenomaneno yanayoendelea na mpaka sasa hivi tayari nimeshaanza kujifunza kushona nguo na nina imani nitakuwa fundi mzuri tu kuliko kutegemea kazi ambayo haina masilahi,” alisema

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
22 Jan 2015

Post a Comment

 
Top