March 16, 2025 02:00:13 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
WAKATI baadhi ya wasanii wa hapa jijini, Dar wakifa huzikwa hapahapa, jambo hilo limekuwa ni tofauti  kwa nyota wa filamu na muziki, Baby Madaha baada ya kufunguka kuwa akitokea amekufa hataki  kuzikwa Dar na badala yake azikiwe jijini, Mwanza.
Nyota wa filamu na muziki, Baby Madaha.
Akizungumza na Uwazi, Madaha alisema kuwa hajui  kifo chake kitatokea lini na anachotaka ni kutimiza yale aliyopewa kama wosia na marehemu baba yake ambaye alizikwa jijini Mwanza. “Nasema ukweli sitaki kuzikwa Dar hasa kwenye makaburi ya Kinondoni, nahitaji kupelekwa nyumbani, wasanii wenzangu wanatakiwa kujua hilo pamoja na ndugu zangu pia, naamini kwamba marehemu baba yangu huko aliko ataona ni vizuri mimi kulala karibu yake kama alivyoniachia wosia huo,” alisema Madah.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
06 Jan 2015

Post a Comment

 
Top