Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Askari Polisi wawili wa kituo cha Polisi Ikwiriri, wilayani Rufiji mkoani Pwani nchini Tanzania wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika waliovamia kituo hicho.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani SACP Ulrich Matei amesema kuwa tukio hilo limetokea saa Nane za usiku wa kuamkia leo ambapo mbali ya kusababisha mauaji hayo watu hao pia wamepora silaha mbalimbali kituoni hapo ikiwemo bunduki SMG 2, Shotgun 1 na SAR 2.
Kamanda Matei amewataja askari waliouawa kuwa ni Edgar Mlinga na Askari wa kike ambaye amefahamika kwa jina moja la Judith na kusisitiza kuwa jeshi la polisi linaendelea na msako mkali ili kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha mbele ya sheria.
Chanzo:-EATV

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top