
Gari aina ya Toyota VX likiwaka moto baada ya kuchomwa na wananchi mchana leo Bunju B jijini Dar kwa kusababisha ajali na kuuwa madereva watatu wa bodaboda...Shuhuda wa Ajali hiyo Amehabarisha kuwa VX ilikuwa katika Mwendo mkali sana Dereva alijaribu kulipita gari la Mbele bila kuwa makini na kujikuta anakutana na Boda bado iliyokuwa imebeba watu watatu (Mshikaki) na Kuwagonga na wote Kufariki Hapo Hapo , Dereva wa XV Hakusimama Japo Tairi la Mbele lilikuwa nimepasuka, Baada ya mwendo kama mita mia sita alisimama na kupaki pembeni na kisha yeye na Abiria aliyekuwa naye kuchukua piki piki na kukimbilia Polisi...Wananchi wenye Hasira walikuta Gari tupu na Kuamua Kulichoma Moto ..

Gari aina ya Toyota VX likiwaka moto baada ya kuchomwa na wananchi mchana leo Bunju B jijini Dar kwa kusababisha ajali na kuuwa madereva watatu wa bodaboda.
Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya gari aina ya Toyota VX imeua madereva watatu wa bodaboda mchana leo.
>>GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment