Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Stori: Gladness Mallya
HUKU akiwa bado hajapona jeraha la kuchanwa usoni na bwana’ke, mwanadada asiyeishiwa matukio Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amefanyiwa kitu mbaya na vibaka na kumnyang’anya kila alichokuwa nacho.

Akizungumza na paparazi wetu, Aunty Lulu alisema tukio hilo lilitokea wiki iliyopita maeneo ya Mwenge, jijini Dar ambapo alikuwa akikatiza mitaa hiyo usiku, vibaka walimvamia na kumpiga maeneo ya usoni na kuanguka ambapo walipata nafasi ya kumuibia simu mbili, saa na pochi iliyokuwa na fedha shilingi 120,000.

Yaani uso wangu umekuwa na manundu kama jambazi niko tu ndani naumwa maana nilipigwa mno, mwaka unaisha vibaya sana kwangu namuomba Mungu huo unaokuja usiwe mbaya kama huu maana ni mwaka wa majanga sana kwangu,” alisema Aunty Lulu.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top