Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
tambwe yanga
Taarifa zilizoingia kwenye mtandao huu dakika chache zilizopita ni kwamba Dar-es-salaam Young Africans imemsajili mshambuliaji wa Simba aliyeachwa Amisi Tambwe .
Yanga imemsajili Tambwe dakika chache zilizopita ambapo anakuja kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Hamis Kiiza ambaye amejiunga na URA ya Uganda .
Tambwe amesajiliwa na Yanga baada ya kuachwa na Simba.
Tambwe amesajiliwa na Yanga baada ya kuachwa na Simba.
Tambwe alikuwa mfungaji bora wa ligi msimu uliopita ambapo alifunga mabao 19 kwenye ligi lakini alishindwa kuwika msimu huu baada ya kutopewa nafasi ya kutosha chini ya Patrick Phiri.
Simba imemuacha Tambwe baada ya kumsajili Danny Serunkuma toka Gor Mahia ya nchini Kenya .
Yanga imekamilisha usjaili huu saa chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa kama ilivyopangwa na Tff .

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top