Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ Penniel Mwingilwa amesema sasa anatamani kuzaa lakini tatizo lipo kwa mwanaume wa kuzaa naye.

 
Penniel Mwingilwa.

Penny alitoa tamko hilo baada ya Diamond kunukuliwa jana (Alhamisi) na gazeti dada la hili, Amani kuwa, alimpa mimba mara mbili binti huyo lakini zikayeyuka katika mazingira ya kutatanisha.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Penny alisema, sasa hivi anapomuona mtoto anachanganyikiwa na kujikuta akitamani naye kuitwa mama hivyo akimpata mwanaume sahihi wa kutimiza ndoto yake hiyo hatafanya ajizi.

“Kiukweli sasa ndiyo ule wakati wa kuzaa, natamani sana mtoto lakini sasa wa kuzaa naye yuko wapi? Hapo ndiyo tatizo maana siyo kuzaa na mtu ili mradi mtoto awe na baba,” alisema Penny.
UNGANA NASI FACEBOOK

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top