Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
HATIMAYE diva wa filamu Bongo, Rose Ndauka ametoa kali ya mwaka kwa kudai kuwa baada ya kutengana na mzazi mwezake sasa hapati tabu tena kwani mama yake mzazi amechukua nafasi hiyo na anampa mapenzi ya dhati ambayo hajawahi kupewa na mwanaume yeyote.
Diva wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
Akizungumza na Uwazi, Rose alisema pamoja na kuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu lakini hakuwahi kupata mapenzi ambayo sasa anapewa na mama yake pamoja na mtoto wake ambao mara zote wamekuwa pamoja.
“Mama na mtoto wangu ndiyo wanaonipa mapenzi ya dhati hakuna wengine, mwanaume hafiki kwenye upendo wa mama, sasa hivi najisikia kuwa huru sana kwa sababu kile nachokihitaji huwa nakipata kwa mama,” alisema Rose.Rose alikuwa akiishi na mchumba wake, Malick Bandawe ambapo waliachana, Septemba mwaka huu.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top