NImsimu wa sikukuu unaendelea! Leo Jumanne najua kila mhusika wa Krismasi yupo moto kuisubiri. Si keshokutwa tu! Oke, ni Jumanne tena ambayo tunakutana wapenzi wasomaji wangu katika safu hii ya maisha ya uhusiano.Wiki iliyopita tuliishia pale mwanadada mmoja aliposema wanaume wanapenda sana kuwaonea wanawake kwa vile wana nguvu ndiyo maana wanawapiga. Sasa tujikumbushe kwanza kisha tunaendelea...
Mwanamke mwingine ambaye nilibahatika kuzungumza naye ni mama Mjori, yeye alisema:
“Kusema kweli hata mimi sipendi kupigwa lakini nimeshawahi kushuhudia mpangaji mwenzangu akipigwa na mume wake kama mbwa kwa mazingira ambayo hata kama mimi ningekuwa ni yule mwanaume ningempiga tu mke wangu.
“Unajua katika ndoa, ikitokea mume amekasirika anaongea halafu na wewe mwanamke unaongea tena kwa sauti ya juu unadhani nini kitafuata hapo.“Wapo wanawake wengine kukiwa na ugomvi wanaongea huku wanatoka nje ili majirani wasikie, hao ndiyo wanaolazimisha kupigwa lakini haiwezekani ukawa chini kwa mumeo akakupiga.”
KUPIGWA BILA KOSA
Kuna kisa kutoka Korogwe, Tanga kinahusu mke aliyewahi kupigwa na mumewe akakimbilia kwa wazazi wake, alipofika akaulizwa nini, akasema: “Mume wangu karudi kutoka kazini akaanza kunipiga.”
Baba mtu akaja juu akisema: “Sasa kama mumeo kakupiga ndiyo unakuja kwangu, unataka na mimi nikupige siyo?”
Mama akaingilia kati kwa kuhoji: “Sasa baba f’lani, mtoto analalamika kapigwa, badala ya kumuuliza chanzo we unamtisha kumpiga tena.”
Baba akajibu: “Sitaki ujinga, mume niliyemuoza huyu binti ana akili timamu, haiwezekani arudi tu nyumbani kutoka kazini na kuanza kumpiga, yeye ndiyo alitakiwa aseme kisa cha kupigwa.”
Alipopewa nafasi ya kujieleza alishindwa kuweka wazi kisa, baba yake akamtaka arudi akaweke mambo yake sawa.
KWAKO JIDE
Judith Wambura Mbibo, yeye ni nyota wa muziki wa kizazi kipya, lakini pia ni mke wa mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Habash. Juzikati ilidaiwa wametengana.Sasa kisa cha kutengana kwao kwa muda mrefu kilikuwa fumbo, ila hivi karibuni ndipo Jide ameamua kuweka wazi kwa kudai kwamba, aliamua kutengana na Gardner kwa vile ndoa yao ilikuwa vipigo kila kukicha!!
Mimi natatizika na madai ya Jide kwani naamini Gardner naye ana akili zake timamu! Je, Jide alikuwa akipigwa kwa ajili ya nini!? Angeweka wazi hapa! Kwamba ilikuwa nikiamka sijaandaa chai mapema napigwa! Nikichelewa kuweka maji ya kuoga napigwa, uwazi ungetufanya tujue udhaifu wa Gardner.
Ni kweli hakuna kosa lolote la kumhalalisha Gardner kumpiga Jide mke wake (kama ni kweli alikuwa akimpiga) lakini isije kuwa Jide yumo kwenye lile kundi la wanawake wanaolazimisha kupigwa!
Hili kundi ndiyo kubwa sana hasa kwa miaka ya hivi karibuni.
Ni kundi linalotokana na wanawake wanaotaka kuwa juu kwenye uhusiano. Ni kundi lenye wake wasiyo na busara wala halina haya! Kwao kuanika matatizo ya ndoa kwa mashoga zao si ishu wala kitu cha ajabu.
Ni kundi ambalo, eti mke naye anataka kukaa baa hadi usiku, mumewe akiwa nyumbani kwa madai ya usawa lakini pia ndilo kundi linaoongoza kwa kutaka kutendewa mema kwa madai ni wajibu wa mume bila kuangalia uwajibikaji wake.
USHAURI WANGU
Kuwa na kusubiriana ndani ya ndoa, kila mmoja awe na hekima za kujua kitu hiki na hapa kilipofika lazima kutulia ili kuzipisha hasira zipite, hapo tutafika mbali!
MWISHO.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro










Post a Comment
Post a Comment