Mtandao wa kijamii wa Instagram, sasa una watumiaji wengi kuliko mtandao wa Twitter.
Instagram inajipanga pia kuboresha huduma zake kwa kufuta akaunti feki.
Instagram, inayomilikiwa na kampuni ya Facebook Inc. (FB), imesema watumiaji wake kwa mwezi sasa wamefikia milioni 300 kutoka milioni 200 mwezi March bila kuhesabu akaunti feki.
Idadi hiyo ni kubwa zaidi kuliko ile ya Twitter ya watumiaji milioni 284 kwa mujibu wa takwimu za mwezi October. Instagram pia itaanza kuwaverify watumiaji wenye majina na brands.
Kila siku watumiaji wapya 360,000 huongezeka kwenye mtandao huo. Instagram imesema kwa wastani watumiaji wake hushare picha milioni 70 kila siku.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment