Kama hukusikiliza Hekaheka ya leo Jumanne ya Desemba 9 kupitia Clouds FM kwenye Leo Tena, inahusu Waumini wa Kanisa la TAG Bukoba kumkataa Mchungaji mpya aliyeletwa Kanisani hapo kwa madai ya kumtaka Mchungaji aliyehamishwa na kupekwa sehemu nyingine arejeshwe.
Baada ya Waumini kumaliza Kuabudu kwa Nyimbo Mchungaji huyo Pius Alphonce aliinuka na kuanza Kuhubiri ndipo baadhi ya Waumini walipoamka na kusema kuwa hawawezi kuendelea na Mahubiri kutokana na watu wachache wanaotaka kulivunja Kanisa hilo kwa maslahi yao binafsi, hivyo kutaka Mchungaji wa zamani Erius Manoti aliyehamishiwa Karagwe arejeshwe.
Hali hiyo ilipelekea mahubiri hayo kusimama na kuzuka fujo na kusababisha ibada hiyo kuahirishwa.
Bonyeza play kusikiliza.
Credit: Millardayo
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment