Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Kivuko kipya cha MV Dar es Salaam-Bagamoyo.
Waziri Magufuli akihutubia wadau waliofika katika sherehe hizo fupi katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa  wa Dar e s Salaam, Mecky Sadick, akizungumza na wadau bandarini.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema  akizungumza jambo.
Baadhi ya wafanyakazi wa bandari wakishuhudia kivuko hicho.

Magufuli na  Sadick wakiwa ndani ya kivuko.
Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko (TEMESA) Japhet Massele, akitoa ufafanuzi kuhusu kivuko hicho.
Waziri Magufuli akionyeshwa kamera na TV zilizomo ndani ya kivuko.
Sehemu ya viti vilivyomo ndani ya kivuko.
Magufuli akikagua moja ya  vifaa vya uokoaji.
Muonekana wa kivuko hiki cha kisasa.
Sehemu ya ndani ya kivuko inavyoonekana.
Magufuli akishuka kwenye kivuko.  Kwa mbali ni boti maalumu ya uokoaji.
... Akiwa na wadau mbalimbali.
KIVUKO kipya kinachotegemea kufanya safari kati ya Jiji la Dar es Salaam na Bagamoyo kimepokelea leo na Waziri wa Ujenzi,John Magufuli katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kivuko hicho mabacho kitakuwa kikipita katika vituo saba kati ya miji hiyo mwili, kimefungwa vyombo vya kuongozea vya kisasa (Navigational Equipment) vikiwemo GPS Compass, Automatic Identification System (AIS), Radar, Echo Sounder, CCTV Cameras na kina vyombo vya kutosha vya kuokolea watu kama ‘life jackets’, ‘life bouys’ na ‘life rafts’.
Akizungumza na GPL, Waziri Magufuli alisema” “Kuanza kwa kivuko hiki kutasaidia kwa kiasi kupunguza foleni kwa wakazi wa jijini la Dar es Salaam, kwani kina uwezo wa kubeba abiria 300 kwa kukaa.

Kujua mengi tembelea www.globaltvtz.com
(NA GABRIEL NG’OSHA/GPL)

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top