Mbeya City imeanza vibaya Ligi Kuu Bara msimu huu kwani inashika mkia ikiwa na pointi tano baada ya kucheza michezo saba, imeshinda mmoja, imetoa sare miwili na kufungwa minne.
Kufanya vibaya kwa timu hiyo kumeibua maneno mengi hasa wakimtuhumu Mwambusi kuwa ameshindwa kazi na ndio sababu uwez wa timu hiyo umeporomoka.
Kutokana na jambo hilo, kocha huyo wa zamani wa Prisons ameamua kuachia ngazi ili kuwapisha wengine baada ya kuchoshwa na maneno mengi yanayoelekezwa kwake.
Mwamabusi aliliambia gazeti hili jana kuwa ameamua kujiweka pembeni ili kuwapisha makocha wengine watakaoweza kuinoa timu hiyo na kuipa mafanikio.
“Maneno ni mengi sana baada ya matokeo haya na wengi wanaelekeza maneno haya kwangu kuwa sifai, mimi mkali, hivyo nimeona bora niwaachie timu yao ili kulinda heshima yangu.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment