Aliyekuwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, YP ambaye amefariki usiku wa jana katika hospitali ya Temeke wakati alipokuwa akitibiwa maradhi ya kifua kikuu (TB) anatarajiwa kuzikwa siku ya kesho katika makaburi ya Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, YP ambaye jina lake halisi ni Yessaya Ambilikile ameugua kwa kipindi cha takribani miezi 2 kabla ya kufikwa na umauti hapo jana.
Hizi ni picha 11 za kutoka eneo la Keko, nyumbani alikokuwa akiishi msanii marehemu ambapo taratibu za mazishi zinafanyika.
Asubuhi ya October 21 Tanzania zilianza kusambaa taarifa za msiba wa aliyekuwa member wa kundi la Tmk Wanaume Family Yp ambaye baadae Meneja wa kundi hilo Said Fella alizithibitisha kwa vyombo vya habari.
Msiba upo maeneo ya Keko Magurumbasi A mahali anapoishi kaka yake Yp,millardayo.com imefika na kuongea na kaka yake huyo ili kujua taratibu za msiba huu zikoje ikiwa ni pamoja na siku ya Mazishi.
John Amulike ambaye ni kaka wa marehemu Yp amesema YP ataagwa kwenye viwanja vya TTC Club Chang’ombe kisha maziko yatafanyika kwenye makaburi ya Chang’ombe.
Yp ameacha Mke na mtoto wa kiume mmoja mwenye umri wa miaka 7.

Baadhi ya waombolezaji
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro




























Post a Comment
Post a Comment