Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Baada ya kusambaa kwa picha ya Ommy Dimpoz anayoonekana akiwa kama kijana wa kijijini aliyetua mjini Dar es Salaam na watu wengi kuhisi ni picha yake ya zamani aliyopigwa wakati anatua Dar (kitu ambacho si kweli), ameamua kuelezea hisia zake.

10706742_760932453944297_1819061735_n
Akiweka picha nyingine kwenye Instagram lakini awamu hii akiwa na Vanessa Mdee (ambayo inaonesha kuwa ni moja ya kazi zake zitakazokuja), Ommy amesema amejifunza mengi kutokana na jinsi watu walivyoiongelea picha hiyo.
10735486_731827086922448_1169205368_n


Ommy na Vanessa Mdee


“Wiki iliyopita nimejifunza mambo mengi sana baada ya ile picha niliyodandia treni kusambaa kwenye mitandao kuna watu waliongelea km utani,kuna watu walinikebehi,wengine waliweka kwenye mitandao na kunitusi kabisa,”ameandika Ommy.
“Ila nilichogundua Sio kila tunachokiona kwenye mitandao kina ukweli tujaribu kuwa wachunguzi,tuache mambo ya kucopy na kupaste jambo la mwisho kabisa siri ya Maisha anaijua mungu usimdharau mtu kwa muonekano unayemuona mshamba eti amekukuta mjini kesho ndo huyo huyo atakayekupa ajira tupendane tusidharauliane……Asante @vanessamdee kwa kupokea na fuko langu.”
Credit Bongo5

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top