Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
ZOEZI la kutafuta miili ya watu waliopoteza maisha kwenye ajali ya mitumbwi katika Ziwa Tanganyika, katika Kijiji cha Kalalangabo Wilayani Kigoma, ambalo lilikuwa likiendeshwa na Vyombo vya Usalama Mkoa wa Kigoma, limesitishwa jana.




Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya, amewaambia Waandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa zoezi hilo limesitishwa jana baada ya kuridhika kuwa hakuna miili mingine inayopatikana.

“Baada ya kuridhika kwamba huenda hakuna zaidi kinachopatikana zoezi la utafutaji zaidi limesitishwa kwa siku ya jana,”alisema Machibya. “Lakini yametolewa maelekezo kwa uongozi wa Kijiji cha Kalalangabo kuendelea kufuatilia na kutoa taarifa mara moja kuhusiana na kuonekana kwa mwili au kitu chochote kwa hatua stahiki.”

Vile vile amevishukuru vyombo vyote vilivyohusika wakati wa zoezi la uokoaji na uopoaji miili ya watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo wakiwemo Waandishi wa Habari, wananchi wa Kijiji cha Kalalangabo na wahudumu wa Afya.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Kigoma, alizungumzia mchakato mzima wa zoezi la uokoaji lilivyokuwa tangu siku ajali hiyo ilipotokea ambapo alieleza kuwa jumla ya watu 10 walipoteza maisha, 25 walipatikana wakiwa salama, watu 11 walipata madhara na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni, ambao kati yao amebaki mmoja anaendelea na matibabu.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya alitoa wito kwa wananchi kuacha mara moja kutumia vyombo vya usafiri visivyo rasmi na ambavyo havijasaliwa kwa kuwa ni hatari kwa usalama.


Octoba 11 mwaka huu mitumbwi ya uvuvi iliyokuwa imebeba maharusi na watu wengine kutoka Kijiji cha Kalalangabo kwenda kijiji cha Kigalye ilipata ajali na kuzama Ziwa Tanganyika umbali wa mita 200 kutoka nchi kavu, ambapo Bwana na Bibi harusi ni miongoni mwa watu walionusurika kifo.


 Credit..Kigomapressclub

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top