Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Staa wa Filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amemlilia rafiki yake kipenzi Sherry Magari aliyefariki dunia hivi karibuni na kusema hana la kufanya zaidi ya kumuombea.


Staa wa Filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’.

Akizungumza na Ijumaa juzi, Mainda alisema alikuwa amejipanga kwenda kumuona jana ‘Alhamisi’ baada ya kusikia kwamba hali yake haikuwa nzuri lakini ikawa imeshindikana kwani kabla ya safari alipata taarifa za kifo chake.
“Nimeumia sana tena sana, yaani dah! Amekwenda rafiki yangu, nilitamani sana kumuona akiwa hai tuongee lakini Mungu akaamua kutenda kazi yake,”  alisema Mainda.

Marehemu Sherry Magari aliyefariki dunia hivi karibuni.

Sherry aliugua ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu na kufikwa na mauti alipokuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.
Kibonajoro.com ndio mtandao wako kwa habari za ndani na nje, Tuwe pamoja huku pia >> Facebook

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top