Mfanyakazi wa Umoja wa mataifa aliesafirishwa mpaka Ujerumani akitokea Liberia wiki iliyopita baada ya kupatwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola, amefariki dunia kwenye hospitali ya St. Georg Ujerumani.
Kifo chake kinamfanya kuwa binadamu wa kwanza kufariki kwa Ebola ndani ya ardhi ya Ujerumani ambapo Mwanaume huyu raia wa Sudan mwenye umri wa miaka 56 alifikishwa kwenye hospitali hiyo akiwa na hali mbaya ambapo amefariki jana usiku baada ya hali yake kuwa mbaya pamoja na kwamba alipewa uangalizi mkubwa wa kupatiwa matibabu.
Msudan huyu aliefariki dunia anakuwa mgonjwa wa tatu wa Ebola kutibiwa nchini Ujerumani sababu tayari kuna Mganda mmoja daktari amekua akitibiwa huko Frankfurt, wakati Yule Msenegal aliruhusiwa kutoka hospitali hivi karibuni baada ya kutibiwa kwa wiki tano.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment