Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Breaking IINajua kama umekua karibu na simu yako leo mitandao ya kijamii hasa Whatsap na twitter inaweza kuwa imetumika kukufikishia Taarifa zilizoanza kuzungumziwa na watu mbalimbali saa kadhaa zilizopita kwamba msanii Chid Benz amekamatwa na Polisi.

Taarifa zinasema kakamatwa na Polisi kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akiwa anaelekea Mbeya na hiyo imetokea baada ya kukutwa na vitu ambavyo ni kosa kwa yeyote kukutwa navyo.
Wakati millardayo.com inaendelea kufatilia hii taarifa kwa upande wa pili wa Polisi, tumezungumza na muandaaji wa show ya Instagram Party ambayo Chid Benz ndio alikua anakwenda kushiriki kesho.
Chidi 1Fred amekiri kweli Chid Benz amezuiliwa na Polisi kwa kukutwa na vitu ambavyo hajavifahamu >>> “Sijapewa taarifa kamili lakini naambiwa kuna tatizo limetokea airport ya Dar es Salaam akiwa anasafiri kuja Mbeya, wameniambia kuna vitu ambavyo amebeba haviruhusiwi kupita Airport
Chidi Benz alikua ameongozana na msanii mwenzake ambae ni Shetta hivyo Chidi kabaki na Polisi na Shetta amekwenda kupanda ndege kwa ajili ya kuelekea Mbeya.
Source Millardayo

Kibonajoro.com ndio mtandao wako kwa habari za ndani na nje, Tuwe pamoja huku pia >> Facebook

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top