Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman.

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, leo amemfuta kazi Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman na nafasi yake kuchukuliwa na Said Hassan Said.

Rais Shein amefanya uteuzi huo wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 55 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984.

Mhe. Said Hassan Said ameteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na uteuzi huo umeaza rasmi leo 7, Oktoba 2014. 

Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu.


Uteuzi wa Mhe. Othman Masoud Othman umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1) na 55 (3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top