Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

MWALIMU wa Shule ya Sekondari ya Muungano iliyopo mji mdogo wa Himo wilayani Moshi, Richard Ndoile (30), anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, kwa tuhuma za kukutwa gesti na mwanafunzi wake wakifanya mapenzi.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita alisema jana ofisini kwake, kuwa tukio la kukamatwa kwa mwalimu huyo lilitokea Oktoba 4, saa 5.00 asubuhi, katika gesti ya Kilimanjaro iliyopo Himo.
 
Moita alisema mwalimu na mwanafunzi huyo (jina linahifadhiwa) ambaye anasoma Shule ya Sekondari Muungano Kidato cha Tatu, walikamatwa baada ya wazazi wa mwanafunzi kumuona binti yao akiwa amepakiwa kwenye pikipiki ya mwalimu wake, kuelekea mahala kusikojulikana.
 
Alisema hatua hiyo iliwafanya kuhamaki na hivyo kuanza kufuatilia mwelekeo wa pikipiki ili kujua hatma ya safari yao hiyo.
Alisema baada ya kuwafuatilia, pikipiki hiyo ilielekea kwenye gesti hiyo na baada ya kuteremka mtuhumiwa na binti yao waliingia ndani na kuchukuwa chumba, kwa lengo la kutimiza haja zao.
 
Kwa mujibu wa Kamanda Moita, wazazi waliamua kupiga simu katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Himo kwa lengo la kutoa taarifa, ambapo polisi walifika lakini hadi mtuhumiwa anakamatwa tayari walikuwa wameshatekeleza tendo la kujamiiana.
 

Alisema mwalimu huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo kidogo cha Himo, kwa ajili ya kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Kibonajoro.com ndio mtandao wako kwa habari za kitaifa/kimataifa, burudani, michezo, udaku na siasa, Tuwe pamoja huku pia >> Facebook , Twitter

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top