
Kutokana na ukweli kuwa tuzo za Grammy zimekuwa zikishutumiwa kwa kutoitendea haki hip-hop, Drake ameamua kufanya alichokifanya H.Baba hivi karibu kwa kuandaa tuzo za Instgram alizoziita ‘Hood Grammys’ na zenye vipengele vitano. Tofauti na H.Baba, Drake hajajipa tuzo yeye mwenyewe.
Rapper huyo mwanzilishi wa label, October’s Very Own (OVO Sound), aliyeshinda tuzo yake ya kwanza ya Grammy mwaka uliopita kwa ‘Best Rap Album’, alitumia Instagram Jumamosi usiku na kutoa tuzo hizo. Kipengele cha ‘Best Vocal Performance of the Year’ kilienda kwa Bobby Shmurda kwa wimbo wake “Hot Ni**a.” “We need it,” alisema Drake.
Kipengele cha ‘Best Performance by a Duo or Group’ kilienda kwa Rae Sremmurd’s “No Flex Zone” na Rich Gang’s “Lifestyle” waliofungana. OG Maco alishinda ‘Best All Around Turn Up’ kwa wimbo wake ‘U Guessed It’ na kumpa msanii wake ‘ILoveMakonnen’ tuzo ya ‘Best Latin Club Anthem’ kwa wimbo wake “Tuesday.”
Msanii wa OVO Sound, PARTYNEXTDOOR alishinda tuzo ya ‘Mixtape of the Year’ kwa, project yake ya PARTYNEXTDOOR TWO. “Grammy’s need to have a rap year. Run it up,” alisema Drake.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment