Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Baadhi ya sehemu za mwili za watu walioungua.
Baadhi ya sehemu za mwili za watu walioungua.




Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam, Mecky Sadick, akiwa na mmoja wa wauguzi wa hospitali ya Temeke alipowatembelea waathirika wa ajali hiyo.
WATU watatu wamefariki na wengine sita  wakiwa katika hali mbaya Hospitali ya Muhimbili kufuatia tukio la moto uliolipuka kwenye gari la kubeba mafuta  jana maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam.
Alizungumza na GPL, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna Mohammed Mpinga, alisema ajali hiyo haikuleta athari yoyote baada ya gari lile kupata ajali ila athari ilijitokeza baada ya watu kuvamia na kuanza kuiba mafuta na baadaye kujaribu kuiba betri ndipo cheche za moto zilipolipuka na kusababisha kuwaka kwa gari hilo.

Wakati huohuo,  Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam Mecky Sadick, amewataka wananchi kutokuwa na tabia ya kuvamia ama kuiba vitu pindi ajali zitokeapo.

Sadick alisema hayo alipotembelea hospitali ya Muhimbili na Temeke walipolazwa majeruhi hao.
Source GPL
Bonyeza Hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top