Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Thomas Eric Duncan mwanaume aliesafiri kutoka Liberia mpaka Marekani akiwa ameambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ebola amefariki muda mfupi uliopita nchini Marekani baada ya kuwa kwenye hali mbaya kwa muda mrefu.
Duncan anakuwa mgonjwa wa kwanza wa Ebola kufariki ndani ya Marekani ambapo Hospitali alikokua amelazwa imethibitisha na kusema ni huzuni kufariki kwa mgonjwa huyu aliepoteza uhai wake asubuhi ya saa moja na dakika 51.
Pamoja na hayo pia mamlaka husika zinaendelea na jitihada za kuhakikisha ugonjwa huo hausambai nchini humo na wanafahamu kabisa kwamba virusi vya Ebola vinaweza kuishi kwenye miili ya watu waliofariki ndio maana wakati wa kuizika ni watu pekee wenye mafunzo maalum tena wakiwa wamejikinga ndio wanaruhusiwa.
Kibonajoro.com ndio mtandao wako kwa habari za kitaifa/kimataifa, burudani, michezo, udaku na siasa, Tuwe pamoja huku pia >> Facebook , Twitter

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top