Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Watoto watatu wa familia moja wamekufa na wengine wanne kujeruhiwa baada ya nyumba yao kumwagiwa petroli kisha kuteketezwa kwa kuchomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kumkia jana.Tukio hilo lililotokea katika mtaa wa Elimu kata ya Kalangala wilayani Geita.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya, Dk. Adam Sijaona, amethibitisha kupokea miili ya watu hao, Mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Ukombozi Reginald Robert (9), Sophia Robert (6) (darasa la kwanza)na Remijius Robert (4).Dk. Sijaona aliwataja waliojeruhiwa sehemu za kifua, kichwani, mikono na miguu na makalio kuwa ni baba wa familia hiyo, Robert Remijius (45), mkewe, Angelina Gaspar (42) na mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Mwatulole, Scolastica Robert (15), aliyehamishiwa hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza kutokana na kuungua vibaya.
BONYEZA HAPA

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top