Paris Hilton hivi karibuni ametumia $230,000 ambazo ni takriban shilingi 379,500,000 kunywa pombe na marafiki zake.
DJ Paris Hilton
Mrembo huyo na washoga zake walitumia $100,000 peke yake kununua chupa kubwa za Ace of Spades Champagne na chupa 11 kila moja za Patrón, Cristal na Grey Goose, kwa mujibu wa mtandao wa Page Six.
Kutokana na bili hiyo, Paris alitoa tip ya $47,000 kwa wahudumu wa kiota hicho ambayo ni zaidi ya shilingi milioni 77. Kwa Hilton, hiyo si fedha ya kuwaza kwakuwa anadaiwa kuingiza dola milioni 2.7 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 4.4 kwa kucheza tu muziki kama DJ kwa siku nne.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment