Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Jamani leo naona mitandaoni hii habari ya Msiba wa Mc Chimamy....

Inauma sana kuona wanawake tunapoteza Uhai wetu kwa sababu ya kuongeza au kuleta uhai wa mtu mwingine, kina mama tunazidi kuweka maisha yetu rehani kwa sababu ya kuongeza rasilimali watu.....yaani mwanamke akipata mimba anaanza kuingiwa na hofu ya kifo.... hata mie nilipokuwa mjamzito nilikuwa napata hofu sana sana.... siyo Haki hata kidogo....

Sitaki kulaumu lakini ifike mahali jambo hili la wanawake kufa kwa sababu ya uzazi lichukuliwe kwa umakini mkubwa na Serikali yetu.....

Mbona kuna nchi ambazo wanawake hawafi kwa sababu ya uzazi???? kwa nini wanawake wa Tanzania tunapuputika in the name of kuzaa?????


Takwimu za vifo vya kinamama kufa kwa sababu ya uzazi ziko juu.... ni lazima ifike mahali kinamama tukatae kufa kwa sababu ya kuleta rasilimali watu.... Ni Lazima serikali iamuke na kutuhakikishia uhai wetu kinamama....
Jamani dada Mc Chimamy Mungu ailaze pema roho yako wewe na mwanao mpz, ambae ulikuwa unamsubiria kwa raha zote....rip my love.....
 
SOURCE-wanawake live
Bonyeza Hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top