Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Bunduki 7 na mabomu 10 yaliyokamatwa huko Bukombe
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa jeshi la polisi mkoani Geita limekamata bunduki saba (pichani) na mabomu 10 eneo la Ushirombo wilaya ya Bukombe.

Inasadikiwa kuwa bunduki hizo ni kati ya bunduki kumi zilizoporwa na majambazi yaliyovamia kituo cha polisi Bukombe na kufanya mauaji ya askari polisi wawili waliokuwa zamu usiku wa kuamkia jana na kujeruhi askari wawili.
Bunduki zilizokamatwa nne ni SMG na tatu aina ya Shotgun pamoja na panga zimepatikana katika tanuru la kuchomea matofali zikiwa zimefichwa pamoja na mabomu hayo.

Habari zinasema kuwa katika msako huo mkali unaoendelea, Jeshi linaloendelea kufanya kazi nzuri limemkamata pia mwalimu mmoja katika shule ya sekondari Ushirombo anayedaiwa kushiriki katika tukio la jana.

Tayari watu wengine watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi.

 Jeshi la polisi linaendelea kufanya msako ili kuwakamata wahusika wote na silaha zote zilizoporwa na majambazi.

Na kwa habari ambazo hatujathibitisha ni kwamba jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha zote na washukiwa watano wanashikiliwa kwa kuhusika na tukio hilo. Endelea kufatilia mtandao wetu habari kamili ikitolewa tutawajuza.
CREDIT:MALUNDE 1

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top