UONGOZI
wa klabu ya Young Africans leo umefanya mkutano na waandishi wa habari
juu na kusema kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu
Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu
isishiriki ni cha kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu
Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu akiongea na waandishi wa habari
leo makao makuu ya klabu ya Yanga, kushoto kwake ni Kocha Mkuu Marcio
Maximo na afisa habari Baraka Kizuguto
Katibu
Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema walipata barua ya mwaliko
wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki
michuano hiyo kwa kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao
kuiwasilisha kwa CECAFA.
Lakini
katika hali ya kushangaza jana tulipokea barua kutoka TFF ikisema
CECAFA imetuondoa kwenye mashindano hayo kwa kushindwa kukidhi vigezo na
kuiteua timu ya Azam kuchukua nafasi yetu "aliongeza Beno."
Kanuni
za CECAFA zipo wazi kuwa wachezaji wanaopaswa kushiriki michuano hiyo
ni lazima wawe na leseni za kucheza mpira kutoka kwa chama husika, jambo
ambalo ambalo orodha tuliyowapelekea wachezaji wote wataichezea Yanga
msimu huu wa 2014/2015.
Kocha
Marcio Maximo alianza maandalizi ya kikosi ambacho kingekwenda
kushiriki michuano hiyo ambayo ilipaswa kuanza ijumaa tarehe 8/8/2014
kwa Yanga kufungua dimba la wenyeji timu ya Rayon FC .
Kikosi
ambacho kocha mkuu alikichagua kwenda kwenye michuano ya Kagame kilikua
na jumla ya wachezaji 20, 15 wakiwa kutoka timu ya kikosi cha wakubwa
na wachezaji watano wakitoka kikosi cha pili U20 chini ya kocha Leonado
Neiva ambaye amekua na wachezaji hao kwa takribani mwezi mmoja.
Lakini
walichokiamua CECAFA ni kuiondoa klabu ya Yanga na kuipa nafasi timu
nyingine kwa kusema kikosi kilichopelekwa hawakubaliani nacho na hata
kocha mkuu Marcio Maximo haendi, hao ndo tulipojua ya kuwa wanataka
majina ya watu na sio timu.
Zifuatazo ni sababu za Kiufundi ambazo Yanga ilizipelekea CECAFA kuhusu kikosi hicho kutojumuisha wachezaji wa timu za Taifa.
a)
Ripoti ya kocha aliyeondoka Yanga msimu uliopita Hans ilitoa maelekezo
ya kupunguza wachezaji tisa (9) na wachezaji wawili kujiunga na klabu ya
Azam hivyo kufanya kikosi kupungua wachezaji 11 kutoka katika idadi ya
wachezaji 30 wa msimu uliopita.
b) Wachezaji 10 wa Yanga wamekuwa na majukumu ya timu za Taifa za Tanzania (Taifa Stars), Rwanda na Uganda tangu Aprili 19, 2014 mpaka mwanzoni mwa Agosti, takribani miezi mitatu wamekuwa kambini bila kupata muda wa kupumzika.
c)
Benchi la Ufundi la Yanga ni jipya kuanzia kocha mkuu Maximo na
wasaidizi wake watatu Leonardo Neiva, Salavatory Edwarda na Shadrack
Nsajigwa hivyo wanahitaji muda wa kuwajua wachezaji waliokuwa kwenye
timu ya Taifa ndo maana hawakuwajumuisha kwenye kikosi cha kwenda Kigali
Rwanda.
d)
Baadhi ya wachezaji wanahitaji Vibali vya kufanyia kazi nchini,
uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili waweza kushiriki michuano ya Kagame, na
moja ya kanuni za CECAFA mchezaji anayeshiriki mashindano hayo ni lazima
awe na leseni ya kucheza mpira kwa ligi ya ndani.
e)
Katika wachezaji 20 waliochaguliwa kushiriki michuano ya Kagame,
wachezaji 6 wamepandishwa moja moja katika kikosi cha wakubwa msimu huu
hivyo kufanya idadi ya wachezaji wa U20 kuwa watano tu.
f)
Wachezaji walikokuwa kambini Taifa Stars kwa takribani miezi mitatu
bila ya kupumzika, daktari alipendekeza wapate japo siku kumi na nne
(14) za kupumzika ili miili yao iweze kupoa na kuanza upya tena
maandalizi ya msimu mpya.
g)
Yanga tunaamini hakuna mtu yoyote zaidi ya Kocha Mkuu anayeweza
kutupangia kikosi cha kwanza, sababu yeye ndio anayekaa na wachezaji mda
wote na kujua ubora wa wachezaji wake.
Chanzo: Tovuti ya klabu ya Yanga sc
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment