Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mwanza. Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa wiki moja, amekutwa ametelekezwa kwenye nyumba ya kulala wageni ya Tupendaene iliyopo Kata ya Buhongwa, Wilaya ya Nyamagana, mkoani hapa.
Wahudumu wa nyumba hiyo walisema juzi kuwa alifika mwanamke aliyekuwa na mtoto mchanga ambaye kwenye kitabu cha wageni aliandika jina la Enjo Festo kutoka Tabora.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, mhudumu Sospeter Joseph alisema wakati wanaendelea na shughuli zao, walisikia sauti ya mtoto akilia kutoka chumba namba moja na walipokwenda, walimkuta peke yake.
Alisema baada ya kutoa taarifa polisi mtoto alichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando kuchunguzwa afya.
Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Benedict Kabadi alisema amepata taarifa za tukio hilo la kinyama, hivyo watahakikisha mhusika anapatikana.
“Kwa kweli tukio hili ni la kusikitisha sana, nimepata taarifa hizo na tumefika eneo la tukio, siyo jambo zuri kwa mtu kumtelekeza mtoto,” alisikitika Kabadi.
  • Bonyeza Hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top