Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This



Mesut Ozil wa Arsenal
Mabingwa wa kombe la F.A nchini Uingereza Arsenal na mabingwa wa ligi ya Uingereza Manchster City wanajianda kutoana jasho kuwania kombe la Charity Shield jioni ya leo  jumapili.
Mechi hiyo ndio itakayofungua rasmi msimu mpya wa ligi kuu nchini humo.


Arsenal itajibwaga uwanjani ikiwa na wachezaji wapya waliosajiliwa kama vile Alexi Sanchez,lakini pia ikikumbuka kichapo cha mabao sita kwa tatu ilichopata dhidi ya mabingwa hao.
Hatahivyo baada ya kushinda taji la F.A kuna motisha kubwa katika uwanja wa Emirates msimu huu.

Yaya Toure Mancity

Frank lampard aliyesaini kandarasi na kilabu ya Mancity kutoka Chelsea hatashiriki katika mechi hiyo .

Vilevile hakuna mchezaji wa kilabu hiyo aliyewasili kutoka likizo ya kombe la dunia wiki iliopita ambaye atashirika katika mechi hiyo huku mshambuliaji Alvaro Negredo akiendelea kuhudumia jeraha lake la mguuni.

Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Goroud huenda akakosa kushiriki baada ya kushindwa kutamba wakati Arsenal ilipochuana na Monaco katika kombe la Emirates.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0712483331.


Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa   

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top