WATU wanne wa familia mbili tofauti, wamepoteza maisha huku wengine wawili wakijeruhiwa katika eneo la Sinai-Mabatini, Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza baada ya kuporomokewa na mawe kufuatia mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na radi usiku wa kuamkia Agosti 17,2014.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentine Mlowola, tukio hilo lilitokea saa 8:55 usiku, ambapo mvua kumbwa iliyoambatana na upepo wa wastani na radi nyingi ilinyesha na kusababisha majabali makubwa ya mawe yanayokadiriwa kuwa na uzito wa tani mbili kuporomoka na kuziponda nyumba hizo.
Aliwataja waliokufa kuwa ni wanafunzi wawili wa shule ya msingi Mbugani, Kefa Joseph (15) na Emmanuel Joseph (12) kutoka katika familia ya Joseph William yenye watu watano, huku mtoto Godfrey Joseph akijeruhiwa na kukimbizwa hospitali.
Kamanda aliitaja familia nyingine iliyoathirika kuwa ni ile ya Samson Odinya ambaye alifariki pamoja na mkewe Kwinta Geko (24) huku mtoto wao, Betty Samson (4) akijeruhiwa.
Tanzania Daima lilifika eneo hilo, saa mbili asubuhi na kuushuhudia nyumba hizo zikiwa zimesambaratishwa kabisa huku nyingine iliyo jirani jiwe likiwa limejikita katikati.
Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya majirani lisema kuwa nyumba zilizofikwa na maafa zinamilikiwa na Joseph William na Lameck Ajiji.
Tukio hilo lilivuta lilivuta hisia za wakazi wengi wa jiji la Mwanza huku wengine wakishindwa kujizuia na kuangua vilio.
Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), alifika eneo la tukio kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoathirika na janga hilo, ambapo alionesha kushtuka baada ya kuelezwa na wananchi kwamba hakuna kiongozi yeyote wa serikali aliyekuwa amefika eneo hilo.
Akizungumza mbele ya umati wa watu waliokuwa wamefurika katika eneo hilo, Wenje alisema; “Inashangaza sana kuona hata mkuu wa wilaya hajafika hapa. Nitawasiliana na viongozi wa serikali na mchana nitarudi hapa tena.”
Mmoja wa wananchi hao, ambaye ni Balozi wa shina namba 5 Mtaa wa Nyerere A, Jackson Kitundu alisema kuwa tukio hilo linasikitisha sana, na kwamba wanaomba viongozi wa serikali wasaidie kuwaondoa wananchi kwenye maeneo ya miamba.
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyeza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment