Picha za staa wa sinema na Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole Kiuno’
zinazomuonesha live akiwa chumbani tena kitandani kimahaba na mwandani
wake, Nuh Mziwanda zimevuja, Risasi Jumammosi linazo kwenye makabrasha
yake.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Shilole, picha
hizo walijipiga wenyewe wakiwa kitandani nyumbani kwa mwanadada huyo,
Kinondoni jijini Dar.
Chanzo hicho kilidai kwamba picha hizo walijipiga baada ya kumalizika
kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani kabla ya hapo
wasingefanya hivyo.
Katika picha hizo zinazowaonesha wawili hao wakiwa katika mahaba niue,
Shilole anaonekana akiwa amemlalia Mziwanda ambaye naye amejiachia vya
kutosha.
‘Shilole’ akipozi kimahaba na mwandani wake, Nuh Mziwanda.
Habari za ndani zinadai kwamba mmoja wa watu wa karibu alishika simu ya
Shilole kisha akajifowadia picha hizo ndiyo chanzo cha kumfikia sosi
wetu huyo.
Baada ya kuzidaka picha hizo, gazeti hili lilimtafuta Shilole ambaye kwa
sasa anakimbiza na ngoma yake mpya ya Namchukua ambapo alipopatikana
kwa njia ya simu alisomewa mashitaka yake ndipo akafunguka namna
alivyochezewa na mtu wa karibu yake.
kimahaba na mwandani wake, Nuh Mziwanda“Kweli hizo picha ni zangu na Nuh
(Mziwanda), tulijipiga kwa ajili ya kumbukumbu na tulikuwa na muda
mrefu hatujiachia si unajua tena Mwezi Mtukufu?
“Unajua simu yangu haina password na nina watu wengi wa karibu so nahisi
ndiyo wamezivujisha na nikimjua namtoa kabisa kwenye network yangu
maana siku nyingine anaweza kunifanyia jambo kubwa baya.”
Mbali
na hilo, Shilole amesema yupo kwenye mazoezi ya kufa mtu akitamba
kwamba atamkimbiza vilivyo staa wa Nigeria, Yemi Alade watakapokutana
jukwaa moja kwa ajili ya shoo kubwa kwenye Tamasha la Usiku wa
Matumaini, Agosti 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
GPL
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:-
0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro










Post a Comment
Post a Comment