Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MTOTO wa umri wa mwaka mmoja amekufa baada ya kutumbukia kwenye ndoo ya maji nyumbani kwao, wakati akicheza. [Image: 1.jpg]
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kihenya wa Kihenya, tukio hilo ni la juzi saa 4:30 asubuhi katika eneo la Buza.

Alisema mtoto huyo, Najma Omary alikuwa akicheza nje ya nyumba yao kulikokuwa na ndoo ya maji na alitumbukia kwa kutanguliza kichwa na kunywa maji mengi yaliyosababisha mauti yake.

Kamanda Kihenya alisema maiti ya mtoto huyo imehifadhiwa hospitali ya Temeke na hakuna mtu anayeshikiliwa na Polisi na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea kufanywa.

Katika tukio la pili, watu 14 wamekamatwa na polisi katika mikoa miwili tofauti ya kipolisi kwa tuhuma za kukutwa na pombe haramu ya gongo pamoja na misokoto ya bangi.

Kamanda Kihenya alisema Polisi waliendesha msako juzi asubuhi maeneo ya Kingungi kwa Nyoka, huko Kiburugwa na kuwakamata watu tisa wakiwa na bangi puri moja na kete 92.

Watuhumiwa hao wanashikiliwa na watafikishwa mahakamani. 
Chanzo maishaforums
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0712483331.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top