Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mtoto Godwin Florence Rweyemamu (3) enzi za uhai wake akiwa na bibi yake, Elda Charles Rweyemamu.
Na Makongoro Oging'
MTOTO Godwin Florence Rweyemamu (3), mkazi wa Kijiji cha Kamala, Kata ya Bangwe mkoani Kigoma aliyeletwa katika Hospitali ya Taifa jijini Dar es Salaam kwa matibabu ya kansa ya macho amefariki dunia leo(jana) asubuhi.

Mtoto Godwin amefariki baada ya kusumbuliwa na kansa ya macho iliyoambatana na malaria na upungufu wa damu mwilini.Godwin aliletwa na bibi yake Elda Charles Rweyemamu katika Hospitali ya Muhimbili hivi karibuni wakitokea mkoani Kigoma kwa ajili ya matibabu lakini uchunguzi wa madaktari uligundua kuwa wamemchelewesha hivyo arudishwe nyumbani Kigoma.
Katika harakati za bibi yake kutafuta nauli ya kurudi Kigoma, wananchi walimchangia shilingi milioni 1.2 ikiwa ni pamoja na tiketi ya ndege na walipaswa kuondoka na Ndege ya Shirika la ATC juzi Jumamosi saa 11 alfajiri, kabla ya muda huo kufika, saa 9 usiku marehemu alizidiwa kutokana na kuishiwa damu pamoja na malaria ambapo alipelekwa Zahanati ya St. Monica, Manzese kisha Hospitali ya Mwananyama, hali ilipozidi kuwa mbaya alipelekwa Muhimbili.
Marehemu anatarajiwa kuzikwa leo Jumatatu katika makaburi ya Mbezi-Makabi jijini Dar.
Bibi wa mtoto huyo ametoa shukrani kwa wale wote waliojaribu kuokoa maisha ya mjukuu wake kwa maombi na michango ya hali na mali.
Kwa yeyote anayependa kuwasiliana na bibi huyo atumie namba  0762 175 1170784 420 215 au 0719 285 100
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyeza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top