Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


STAA wa filamu za Kibongo, Deogratius Shija ameugua ghafla na kulazwa katika hospitali moja jijini Johannesburg, Afrika Kusini alipokwenda kwa mapumziko mafupi.
Akiwasiliana na mwandishi wetu kupitia mtandao mmoja wa kijamii, rafiki wa karibu wa Shija aliyeomba hifadhi ya jina lake alithibitisha kuhusu kuugua kwa msanii huyo.
Ni kweli Shija amelazwa hapa Kwazulu Natal, aligua ghafla kutokana na mbadilishano wa hali ya hewa.


Hapa Sauzi kipindi hiki kuna baridi kali sana. Kwa huko Bongo, unaweza kufananisha na Mufindi, lakini hali yake siyo mbaya sana, anaendelea vizuri
alisema rafiki huyo ambaye ndiye mwenyeji wa Shija.
Siku ya pili, mwandishi wetu alifanikiwa kuwasiliana na Shija kupitia mtandao mwingine wa kijamii ambapo alisema:
Ni kweli kaka nilipata dhoruba la afya kidogo, lakini nashukuru sasa nipo poa na nimeshatoka hospitalini.

box;">UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
 

 kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top