Wananchi wakitazama eneo la tukio |
Kijana mmoja aitwaye Daniel John (30) Muha mkulima na mkazi wa Majengo Kahama ameuawa kwa kupigwa mawe na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na wananchi waliojichukulia sheria mkononi baada ya kutuhumiwa kuiba/kutapeli pikipiki.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa sita mchana katika mtaa na kata ya Nyihogo mjini Kahama, eneo la Mnazi Mmoja, Barabara ya Tabora Karibu na Ofisi za halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga.

Gari la Polisi likiondoka eneo la tukio baada ya kuuchukua mwili wa Marehemu |
Taarifa zinadai kwamba mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa ni marehemu inadaiwa alikodisha Pikipiki hiyo zaidi ya Miezi mitatu iliyopita katika eneo la Maegesho ya Daladala za Pikipiki katika Lango kuu la hospital ya Wilaya hiyo.
Aidha Mmiliki wa Pikipiki hiyo ambaye hajafahamika mara moja wala namba ya pikipiki, inadaiwa alimkamata mhutuhumiwa maeneo ya mtaa wa Shunu Kata ya Nyahanga ambapo aliamua kumpeleka katika kituo cha polisi akiwa amemfunga kamba.

Imeelezwa kuwa baada ya wananchi kuona mtuhumiwa amefungwa kamba ndipo wakamuuliza mmiliki huyo ambaye aliwaeleza, na ghafla wananchi wakaanza kumshambulia kwa mawe na kisha kumchoma Moto.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SSP Longinus Tibishubwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mara baada ya mauaji hayo wananchi na mmiliki wa pikipiki walitoweka na pikipiki hiyo na kwemda nayo kusikojulikana.
Kamanda Tibishubwa amesema jeshi la polisi linaendelea na msako mkali kuwabaini na kuwakamata wahusika wote wa mauaji hayo sambamba na mmiliki wa pikipiki hiyo.
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahusika wa mauaji hayo.
Aidha ametoa hamasa kwa wananchi kuacha mara moja tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni ukiukwaji wa sheria za nchi na haki za binadamu.
Na malunde1 blog
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyeza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment