Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwanamke (kikongwe)anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 85 hadi 90 amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani juu ya mti karibu na nyumba yake katika mtaa wa Busalala kata ya Kizumbi tarafa ya Shinyanga mjini katika manispaa ya Shinyanga.

Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Longinus Tibishubwa amesema tukio hilo limetokea jana saa sita mchana.

Amesema mwili wa marehemu uligunduliwa na mjukuu wa kikongwa huyo aitwaye Asia Muhammed huku akiongeza kuwa chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa.
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyeza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top