
Mganga maarufu wa kienyeji, Dr. Manyaunyau ametoa msaada wa kusambaza maji bila kurudishiwa gharama yoyote kwa wakazi wa wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani.
Akiongea
na Sunrise ya 100.5 Times Fm, Dr Manyaunyau amesema ameanza kutoa
huduma hiyo muda mrefu lakini hakujitokeza kwenye vyombo vya habari
kueleza kwa kuwa nia yake haikuwa kujitangaza, hadi pale alipofuatwa na
kipindi hicho na kuamua kuwaeleza watanzania.
Mkuu
wa wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila amethibitisha kuwa Manyaunyau amekuwa
akitoa msaada huo na kwamba serikali kwa upande wake pia imekuwa
ikiendelea na zoezi hilo kwa upande mwingine.
Nao
wakazi wa Mkuranga wameelezea kuwa hivi sasa wanatumia zaidi maji
yaliyosambazwa na Dr Manyaunyau kwa kuwa maji yanayosambazwa na
halmashauri ya Mkuranga yamekuwa yakikatika kwa muda mrefu.
“Kwa
kweli halmashauri ya Mkuranga tuna shida sana ya uhaba wa maji kutokana
na kwamba tuna mabomba lakini mabomba mengi hayatoi maji. Maji
yanayotumika sana ni ya Dr Manyaunyau, ambaye amesambazasambaza Mkuranga
na watu wengi wameweka mabomba na wanapata maji majumbani mwao. Lakini
kwa maji ya halmashauri, karibu miezi miwili mitatu maji hayatoki na
yakitoka ni ya mgao. Yakitoka leo kesho hayatoki.” Amesema Mkazi wa
Mkuranga.
Tovuti
ya Times Fm ilizungumza na Dr Manyaunyau muda mfupi baadae na kikubwa
tulitaka kufahamu gharama alizotumia kusambaza maji.
“Nilianza
mdogomdogo lakini mpaka sasa hivi kwa tathimini ya haraka ya mradi
wangu unafika mpaka kwenye 50 milioni, kwa kukadiriakadiria hivi inaweza
kufika.” Amesema Manyaunyau.
Akieleza
kuhusu idadi ya watu aliowasambazia maji katika wilaya hiyo, Manyaunyau
ambaye mbali na kuwa mganga ni mfanyabiashara amesema yeye hufanya tu
na hajakaa bado kuanza kuzihesabu kaya alizozihudumia.
Ameeleza
kuwa lengo lake hasa ni kuhakikisha anaweza pia kuisaidia jamii kwa
kiasi anachokipata kwa kuwa amejali kupata kutoka kwenye jamii hiyo
hiyo.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment