Hitmaker
wa nyimbo kama Barua,Mume Bwege na Dunia Njia, Ruta Bushoke ambaye kwa
sasa anaishi nchini Afrika Kusini, anatarajia kuachia wimbo mpya na
album.
Bushoke ambaye anaishi jijini Pretoria, ameiambia mdadisiblog kuwa kwenye album hiyo amemshirikisha baba yake Mzee Max Bushoke aliyewahi kuwa mwanamuziki wa bendi ya Sikinde huku kwa sasa akifanya kazi ya utangazaji nchini humo.
“Album yangu mpya ambayo nimemshirikisha Baba Mzee Max Bushoke inaitwa Bushoke international Album,” amesema Bushoke. “Nimemshirikisha katika nyimbo kama 3.
Bado haijaisha. Ila nyimbo kama 8 zipo tayari Ukiacha ‘She Want It’ niliyofanya na Face off kutoka Uganda. Kwa sasa “Bwagamoyo” ndio nyimbo rasmi ntaitambulisha nimeimba peke yangu. Nimefanya katika studio inaitwa Tidy Production Cape Town, producer ni Danro. Na pia nimeshafanya video za ngoma kama tatu pamoja na hii ya Bwagamoyo.”
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment