Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This



Arsenal wanasubiri matokeo ya vipimo vya pili vya scan vya Olivier Giroud baada ya kuumia kiwiko cha mguu, na huenda akakosa kucheza kwa miezi mitatu.
Giroud, 27, aliumia katika mchezo dhidi ya Everton uliomalizika kwa sare ya 2-2.
Alitakiwa kufanyiwa vipimo vya pili kuona madhara aliyopata baada ya uvimbe kupungua.
Kukosekana kwa Giroud kunamaanisha Alexis Sanchez, Joel Campbell, Yaya Sanogo na Lukas Podolski, ndio tegemeo la ushambuliaji.
Sanogo hata hivyo ana jeraha la msuli na huenda asiweze kucheza mechi ya Champions League dhidi ya Besitkas siku ya Jumatano.
Bonyeza Hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top